HomeResourcesSabbath School quarterly

Utomvu

02/04/2026

Kukaa ndani ya Kristo wakati mwingine kunaweza kuonekana kama moja ya mambo magumu zaidi kufanya. Tunaweza kujua kwamba hiki ndicho, tunachohitaji, lakini, hekaheka za maisha hutuvuta kwenye mkondo wake, na kisha inaonekana kuwa vigumu sana. Kumfuata Mungu kunaweza kuonekana kuwa mzigo mkubwa zaidi kuwahi kutokea, hasa kwa wale wanaoudhiwa na mtu anayejaribu kuwafanya wamfuate Yesu. Dini ya aina hii inaweza kuonekana kuwa ya kuchosha kwa sababu yote huwa inahusu matendo ya nje badala ya yale yaliyo moyoni. Hakuna kinachoweza kuwa mbali zaidi ya kile ambacho Mungu anatamani, ambao ni uhusiano ambao msingi wake ni upendo wa pande zote, si sheria tu; uhusiano uliochaguliwa (ambamo Yeye alikuchagua wewe kwanza) kulingana na upendo na uchaguzi wa bure.

Wakati mwingine tunaweza kuwa tumeunganishwa kwa kiasi fulani na Mzabibu lakini hatujakaa kweli kwa kila nyuzi za utu wetu. Tunaweza kwenda kanisani, kuomba na kufanya kile tunachojua ni sawa, lakini ndani tunahisi kudhoofika. Ukweli ni huu: Hatuwezi kujiweka wenyewe ndani ya Yesu kama vile tawi lisivyoweza kujiunganisha lenyewe na mzabibu. Mungu alitupenda sisi kwanza; Alifanya hatua ya kwanza. Mwitiko wetu daima ni mwitikio kwa kile ambacho Mungu ametufanyia kwanza.

Ikiwa unatazama jinsi mzabibu unavyoishi wakati, wa majira ya baridi, utajifunza ukweli wa kuvutia - machipukizi kwenye matawi hupungukiwa na maji na kutengwa na mfumo wa kukua hadi majira ya kuchipua. Wakati udongo unapopata joto, mizizi hufyonza maji, na utomvu hupanda kupitia shina la mzabibu hadi kwenye machipukizi na kisha huanzisha ukuaji. Bila utomvu unaotiririka kupitia katika mzabibu, hakuna ukuaji utakaotokea.

Utomvu katika mzabibu ni kama Roho Mtakatifu maishani mwetu. Tunaweza kuwa kama tawi lililokufa, lakini tunapochagua kutumia muda pamoja na Mungu, Roho Mtakatifu humiminika ndani yetu, kama utomvu kutoka kwenye mizizi na kutuleta kwenye uzima ili tuanze kukua. Vilevile tunahitaji kufanya uamuzi wa kutaka kukaa ndani ya Yesu, ni lazima pia tuombe Roho Mtakatifu (utomvu) atiririkie maishani mwetu.

Kwa kweli ni Roho Mtakatifu anayeleta ukuaji na kuhakikisha kwamba tunastawi na kushikamana na Mzabibu. Tunahitajika kila siku kwa ajili ya Roho Mtakatifu, ambaye yuko pamoja nasi hapa duniani ili:

  • Awe Msaidizi wetu (Yohana 14:16-18).
  • Amfunue Yesu kwetu (Yohana 15:26).
  • Atusadikishe kuhusu dhambi (Yohana 16:7, 8).
  • Utuongoze katika kweli yote (Yohana 16:13).