HomeResourcesSabbath School quarterly
Jifunze zaidi
03/04/2026
Kabla hatujazaliwa, Mungu alitupenda; Alipanga kutujua na sisi tumjue Yeye. Anatutafuta, kama Mchungaji mwema, na anatualika kukaa ndani Yake kila siku. Tunahitaji tu kuchagua kumwitikia Yeye, na kisha kubadilisha unyonge wetu na hali yetu ya u - Laodikia kwa zawadi zake nzuri (taz. Ufu. 3:18, 19).
Kama ulivyo ukuaji wa polepole wa matawi ya mzabibu, uhusiano wetu na Mungu unaweza kukua polepole, au unaweza kulipuka na kufurika kutokana na mvua tunayohitaji sana. Bila kujali kasi tunayokua nayo na wingi wa matunda yanayozalishwa katika maisha yetu, tunahitaji “utomvu” wa kila siku, au Roho Mtakatitu, ili kuhakikisha kwamba tunabaki tukishikamana na Yesu.
“ 'Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu.’ Kukaa ndani yake Kristo kunamaanisha kudumu kumpokea Roho wake Mtakatifu. Maisha ya kujisalimisha kindakindaki katika huduma Yake. Njia ya mawasiliano ni lazima iwe wazi kila mara kati ya mwanadamu na Mungu wake. Kama matawi ya mzabibu ni lazima sisi tushikamane na Yesu na kupokea nguvu na tabia yake kamilifu kwa imani.” — Ellen G. White, Tumaini la Vizazi Vyote, Sehemu ya Pili, uk. 290.
“Mche mkavu uliokatwa unawezaje kuwa mmoja na shina la mzabibu kuu? Unawezaje kufanywa kuwa sehemu ya maisha na ustawi wa mzabibu ulio hai? Ni kwa kupandikizwa tu ndani ya mzabibu, kwa kuletwa kwenye uhusiano wa karibu zaidi iwezekanavyo. Nyuzi kwa nyuzi, mshipa kwa mshipa, tawi hushikilia sana mzabibu unaotoa uhai hadi uhai wa mzabibu, kama tawi hilo likiwa na tawi.” — Ellen G. White, Manuscript 67, 1897.
Masawali ya Kujadili
Muhtasari: Kabla ya kuanza kukua katika uhusiano na Mungu, inatubidi kwanza kutulia ili kufikiria uhusiano wetu wa sasa na Yeye ulivyo. Ikiwa ni Laodikia au ikiwa matawi yetu hayastawi, Yesu ana suluhisho kamili kwa hali yetu ya kiroho: kukaa ndani Yake.