HomeResourcesSabbath School quarterly

Katika Umilele

20/06/2026

Somo la Juma Hili

Zaburi 80, 1 The. 4:17, Ufu. 21:9-27, Isa. 25:8, Ufu. 7:17, Ufu. 21:4, Yn. 6:44.

Fungu la Kukariri

Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo (#1 Yoh. 3:2#).

Wakati ujao una nini kwa ajili yako? Ni kitu gani kipo huko mbele? Unaweza kuwa wa kutisha, wa kusisimua, wa kuogofya, na wa kushangaza, vyote kwa wakati mmoja. Jua kwamba Bwana Yesu ni mwaminifu na kwamba maneno Yake ni ya kweli (Ufu. 3:14). Bado zitakuwepo siku za dhoruba hapo mbele (Mt. 24:21, 22), lakini ameahidi kwamba kamwe hatakupungukia kabisa, wala kukuacha (Ebr. 13:5). Yeye atatenda hakika kile alichosema atakitenda — daima ametenda Naye daima atatenda (Ebr. 10:23). Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka (Mt. 24:13).

Bila kujali idadi ya siku tulizobakiza duniani, yatupasa tukaze macho yetu kwa Yesu, tukidumu bila kuchoka kumtazama Yeye. Hili sio rahisi siku zote katika ulimwengu unaong'ang'ania kusikilizwa, lakini hebu sisi, kama Daudi, tuseme, “Macho yangu humwelekea Bwana daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu” (Zab. 25:15).

Juma hili, hebu tujifunze kuhusu zawadi ya mbinguni (Mt. 5:12; Ufu. 22:12); jinsi mbinguni patakavyokuwa; na hatimaye, itakavyopendeza kuwa pamoja na Yeye aliyetuumba, aliyetupenda hadi mauti, ambaye ametukomboa kutoka katika dhambi, Naye anakuja tena upesi. Inatupasa kushikilia kile tulicho nacho kwa Imani hadi wakati huo.

Jifunze somo la juma hili kwa maandalizi ya Sabato ya Juni 27.