HomeResourcesSabbath School quarterly
Muda
26/04/2026
Je umewahi kutega kamsa ili itoe mlio mapema kabla ya muda wa kawaida ili kukuamsha upate kusoma Biblia yako? Umewahi kujitahidi kujivuta kutoka kitandani na kisha ukatazama saa na kufikiri, “Ninazo dakika kumi na tano kabla sijaanza shughuli za siku. Yanipasa niharakishe! Umewahi kupitia msongo unaokufikisha katika kuwa na ombi fupi au kupitia sura ya Biblia juu juu tu, na kujikuta ukiridhisha dhamiri yako huku ukiuacha moyo wako katika hali ya kutoridhishwa na matokeo kabla ya kukimbilia katika hekaheka za siku?
“Lakini kuna faida ndogo katika kusoma Biblia kwa haraka haraka. Mtu aweza kusoma Biblia yote na bado akashindwa kuuona uzuri au kufahamu maana zake za kina na zilizojificha.” — Ellen G. White, Jipatie Amani Moyoni, uk. 68.
Ingawa kwa hakika kuna baraka zinazotokana na kusoma Biblia—kama vile kunywa kutoka kwenye bomba la kuzima moto (kwa wingi na kwa haraka)—inawezekana kusoma Biblia kwa haraka na bado ukakosa mengi sana. Mungu alitupatia Neno Lake lililovuviwa, la thamani, ili tupate kujua mengi zaidi kumhusu (na, katika mchakato huo, zaidi kuhusu sisi wenyewe, pia). Tunapochukua muda kuona tabia isiyoelezeka iliyo nzuri, ya Mungu na njia ambazo Ameingiliana na wanadamu katika historia, tunaweza tu kumpenda Yeye zaidi. Rekodi ya mwingiliano Wake iko pale pale mikononi mwetu—lakini lazima tupate muda, na tuchukue muda, kumjua Mungu kupitia kusoma Neno Lake (Mdo. 17:11). Fikiria mapendekezo yafuatayo:
Mwombe Mungu akuwekee shauku moyoni mwako kwa ajili Yake. Dai ahadi katika Yeremia 29:13 na Zaburi 37:4. Mwalike akuamshe mapema kuliko kawaida au akupe muda katika siku yako kufanya hivyo.
Salimisha muda wako kwa Mungu. Ndiyo, una shughuli nyingi, na kuna mambo mengi ya haraka ya kufanya. Lakini wakati na Mungu ni wa thamani sana. Nenda mahali tulivu peke yako na usome Zaburi 46:10. Soma maneno au mwimbie Mungu wimbo “Yote namtolea Yesu.” Fikiria juu ya maeneo ya maisha yako ambayo hayawezi kusalimishwa nawe uyatoe kwa Mungu.
Tumia muda na Mungu hata kama haujisikii kufanya hivyo. Kama vile inavyohitajika kuchagua kwa uangalitu na kuwa na mpango wa utekelezaji ili kuwa na afya njema (mazoezi, kula vizuri), uamuzi wa makusudi unahitajika kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu. Kumbuka kwamba kujenga mazoea mapya kunaweza kuchukua angalau siku 21, na hatuwezi kamwe kufaulu bila msaada wa Roho Mtakatifu.