HomeResourcesSabbath School quarterly
Kujifunza Biblia kwa Kina
28/04/2026
Hata kama wewe sio mtaalamu — mwanazuoni ili ujifunze Biblia, unawezaje kujifunza Biblia kwa kina?
Omba: Haiwezekani kutilia chumvi umuhimu wa maombi kama vilivyo vishikiza vitabu kwa (na vialamisho kote) kuhusu muda wako wa kujifunza Biblia. Ellen G. White anatuambia kwamba tunapokuja kusoma Biblia, hatuko peke yetu. Kwa kumwalika Roho Mtakatifu kuwa kiongozi wetu, tunakataa vikengeusha-fikira vingine vyote, na adui hukimbia. “Kamwe Biblia isijifunzwe bila maombi. Roho Mtakatifu pekee Ndiye anaweza kutufanya tuhisi umuhimu wa mambo yale ambayo ni rahisi kueleweka, au kutuzuia tusianze kupotosha ukweli ambao ni mgumu kwetu kuuelewa.” —Pambano Kuu, uk. 494,
Soma na Uandike: Inaweza kusemwa kwamba tofauti kuu kati ya kusoma Biblia tu, na kuisoma, inakuja kwenye tendo moja kuu: kuandika. Kuandika hutusaidia kupunguza kasi ya mawazo yetu, kutafakari Neno la Mungu, na kulipitia kwa mwendo utakaowezesha uchunguzi, ufasiri, matumizi, na uwajibikaji unaoweza kutokea. Vilevile huwa kufanya hivyo kunasaidia mawazo yetu ya awali yaliyotawanyika kujifanyia kazi yenyewe —kutoka kichwani, hadi kwenye kalamu yetu, na kisha uingia mioyoni mwetu kwa siku hiyo. Pia tuna uwezekano mkubwa wa kukumbuka jambo ambalo tumeandika (Zab. 119:15, 16). Ikiwa huwezi kuandika, jaribu kusoma Biblia kwa sauti (au kuisikiliza), ikifuatiwa na mawazo yako kama sala kwa Mungu.
Shiriki: Mwambie mtu mwingine kile ambacho umejifunza. Hiki kitaiimarisha akilini mwako na kumtia moyo mtu mwingine.
Kwa kuanzia, chagua kitabu kifupi cha Biblia (kama vile Yona, Marko, Wafilipi, au 1 Yohana), kisha taratibu upitie kitabu hicho. Huu ni mtazamo sahili unaoweza kuutumia kwa fungu moja (mbinu ya aya kwa aya), ibara, au sura nzima:
- Omba ili Roho Mtakatifu aongoze akili yako na kulainisha moyo wako unapokuwa ukisoma.
- Chagua aya au ibara ya Biblia.
- Andika ibara husika au sehemu za ibara zinazojitokeza kwa hoja nzito kwako kwenye shajara au daftari.
- Isome ibara kwa maombi na upigie mstari mawazo makuu.
- Andika kile unachokipata kutoka kwenye mawazo uliyoyapigia mstari.
- Ombea mawazo haya na jinsi yanavyogusa uhusiano wako na Mungu.
- Mfikirie yule utakayeweza kumshirikisha haya leo.
“Wakati wowote watu wa Mungu wanapokuwa wakikua katika neema, watadumu katika kupata uelewa ulio wazi zaidi wa Neno Lake. Wataitambua nuru mpya na uzuri katika ukweli wake. Huu ndio umekuwa ukweli katika historia ya kanisa katika vizazi vyote, na ndivyo utakavyoendelea hadi mwisho.”_ — Ellen G. White, Counsels to Writers and Editors, wk. 28, 39._