HomeResourcesSabbath School quarterly

Vishawishi na Majaribu

24/05/2026

Pambano kuu ni halisi, Sisi sote tunahusika ndani yake, Vita ya ulimwengu wote iliyoanza mbinguni sasa inapiganwa katika maisha ya kila mmoja wetu, pia.

Shetani anajua kwamba anapaswa kutumia kila alicho nacho katika zama hizi tunazoishi, kabla tu ya Yesu kurudi, ili kutuzuia kuwa na uhusiano na Mungu. Huenda umeshawishiwa na kitu ambacho si lazima kiwe kibaya kwa chenyewe lakini kinakuchukulia muda mrefu na nguvu nyingi kiasi kwamba vinabakia kiasi kidogo mno kwa ajili ya Mungu. Huenda ni kazi, mitandao ya kijamii, manunuzi, michezo, au chakula. Tunapojichunguza kwa makini, tutaona kwamba matumizi yaliyopita kiasi na hali ya kukosa uwiano chochote cha vitu hivi, kunaweza kusababisha kuwe na muda kidogo tu kwa ajili ya Mungu na wengine. Adui anajua kila aina ya udhaifu wetu na aina ya vitu ambavyo vinatushawishi kutotumia muda na Mungu. Imetupasa kukumbuka kumtafuta Mungu kwanza (Mt 6:33) kabla ya kuharakisha kuingia katika siku yetu na yale yote yanaweza kutujia.

Yesu anajua hali yetu, lakini anakemea kutojali kwetu (Ufu. 3:14-22). Ingawa Yeye ni Mungu, pia alikuwa binadamu aliyeweza kuchoka, kama ilivyo kwetu (Yn. 4:6). Alijua shinikizo za maisha, kama tujuavyo, lakini mara nyingi alipata ahueni kwa kwenda mbali mwenyewe kuomba kwa Baba Yake (Luka 5:16, Luka 6:12, Marko 1:35, Mathayo 14:23). Alijua kuwa muda wa kuwa na pamoja na Baba yake kilikuwa kitu bora zaidi ambacho alipaswa kufanya ili kurejesha nguvu ya kupambana na majaribu. Ni kitu bora na njia ya uhakika kabisa kwetu sisi pia.

Samsoni alianguka kwa sababu alidhani alikuwa na nguvu. Alitegemea nguvu zake mwenyewe kushinda majaribu. Kila siku kila mmoja wetu anakabiliana na mapambano na dhambi kadiri adui wa roho zetu anavyojaribu kudhoofisha na kuharibu uhusiano wetu na Mungu. Anajua udhaifu wetu na anaweka nguvu katika maeneo hayo ili apate kudhoofisha uhusiano wetu na Mungu na kuleta hatia na hisi ya kutostahili mioyoni mwetu ambavyo vyote vina mwelekeo wa kutusukuma kwenda mbali na Mungu. Mwovu anafanya kazi kuhamisha fikra zetu, makusudi yetu na matendo yetu ili apate ngome katika baadhi ya sehemu za maisha yetu. Lakini kumbuka, imani yetu itatusaidia kusimama na imani huja kwa kusikia Neno la Mungu.