HomeResourcesSabbath School quarterly
Kujua na Kutenda
28/05/2026
Katika Hubiri la Mlimani, Yesu anazungumza mno juu ya uhusiano—Naye na uhusiano wa kila mtu na mwenzake. Anasema Kitu ambacho kinagusa sana moyo kuelekea mwisho wa ujumbe Wake.
“ Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni ” (Mt. 7:21).
Yesu anaeleza kwamba wengine watamwita na kwa bayana kujua habari Zake bila kumjua hasa. Bila shaka, kutafuta maarifa ni muhimu, na Biblia inatuambia kwamba watu wa Mungu wangeweza kuangamia kwa kukosa maarifa na kwa sababu wamekataa maarifa yao juu yake (Hosea 4:6,10). Kamwe hatupaswi kupuuza umuhimu wa kweli za Biblia zisizopitwa na wakati. Lakini ikiwa maarifa hayo hayatubadilishi na kuimarisha uhusiano wetu na utembeaji wetu na Mungu, hauna manufaa.
“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma”(Yn 17:3). Yesu alisema kuwa kigezo cha lazima cha kuingia mbinguni ni kufanya mapenzi ya Mungu na hatimaye kumjua Mungu — kwa vile hatuwezi kufanya mapenzi Yake pasipo kumjua. Hiki ndicho kigezo cha msingi na matarajio ya maana sana. Ikiwa watoto wako watasema wanakupenda na kwa kawaida wanatenda yale unayowataka, matendo yao yanafunua kina cha upendo wao na heshima yao kwako. Vivyo hivyo, tukimpenda Mungu tutataka kufanya mapenzi Yake, kwa vile tunajua kuwa hakuna kitu bora zaidi ya hayo kwetu sisi kufanya! Mwitiko wetu Kwake, na hatimaye utii wetu Kwake kama mtiririko wa upendo wetu huonesha jinsi uhusiano wetu ulivyo hasa.
Tutakapousikia hasa ujumbe wa Yesu, lazima tutapata changamoto na kubadilika. Lakini, kwanza kabisa, masikio yetu sharti yafunguliwe na mioyo yetu iwe yenye kupokea ili kwamba mpango makini kwa ajili ya kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu uweze kukaziwa katika roho zetu wenyewe kwa kila pumzi tuvutayo. Maisha yetu yanaweza kujengwa juu ya mwamba, na mpango mkamilifu wa Mungu kwa ajili yetu.