HomeResourcesSabbath School quarterly
Sheria
26/05/2026
Dhambi ni uvunjaji wa sheria ya Mungu (1 Yohana 3:4) na dhambi pia imo ndani ya asili zetu (Zab. 51:5; Yer. 17:9). Kwa hiyo ni sheria inayofanya tuelewe kile hasa dhambi ilicho. Sheria ni kama kuvaa miwani ili kwamba tuweze kuona vizuri kile kinachotuzunguka au kutumia kioo kuona vile tunavyoonekana. Inaleta ufasaha na usadikisho katika maisha yetu na tabia zetu na wakati huo huo ikituambia juu ya tabia ya Mungu na kile kilicho muhimu Kwake.
Amri kumi (Kut. 20:3-17) ziliandikwa kwa chanda cha Mungu. Yesu alisisitiza umuhimu wake: “nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi” (Mk. 12:30-31). Aliongeza: “Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii” (Mt 22:40).
Maneno ya Mungu kwa Waisraeli katika mlima Sinai na kwetu leo (Ebr. 1:1,2) yanatuambia kwamba jukumu la sheria hasa ni uhusiano. Mungu alitoa sheria kama kinga ili kulinda uhusiano wetu Naye pamoja na uhusiano wetu na wengine. Hata hivyo, Shetani ameharibu uzuri wa sheria ya Mungu kiasi kwamba wengine wanaiona kama mzigo. Ushupavu wa sheria badala ya upendo na uhuru mara nyingi unahusianishwa na sheria, hata kama Biblia inatuambia, “‘Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito’ ” (1 Yoh 5:3).
`1. Katika kipimo cha moja hadi tano, Neno Lililohai ni la thamani kiasi gani (na sheria kama sehemu yake)
-
Ninaposhika sheria ya Mungu, je, inanidhibiti au inanitia nguvu? Ninawezaje kuielewa vyema sheria ikiwa ninadhani inanidhibiti?
-
Ni nini kinaweza kutokea ikiwa sheria ya Mungu ya upendo Kwake na wengine ingeletwa katika kiini cha maisha yangu, familia yangu na kanisa langu? Ni kitu gani kitapaswa kubadilika katika maisha yangu na uhusiano wangu?`