HomeResourcesSabbath School quarterly
VIKWAZO
06/06/2026
Somo la Juma Hili
Marko 4:35—41; Marko 5:21-34: Rum. 5:3-5 Ayu. 19:23-27; Ayu. 23:8-12; Luka 24:13-27; Rum. 8:18,
Fungu la Kukariri
“Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi” (#Warumi 5:3-5#).
Jioni moja, jua lilipokuwa likizama kwenye upeo wa macho, msichana alikuwa akitembea kuelekea nyumbani wakati dhoruba nzito ilipoanza kuvuma. Aliongeza mwendo, akijua bado kuna umbali wa kutembea. Tone moja la mvua lilidondoka shavuni mwake, kisha lingine, na ghafla, alikuwa ameloa chepechepe. Akaanza kukimbia kuelekea mlango wa mbele wa nyumba yao, ambapo baba yake alimkimbilia kumlaki. Alikuwa akimtazama kutoka dirishani. Alipomfunika kwa blanketi mabegani mwake, akamwuliza, “Nilikuona sasa hivi tu, kwenye mvua. Kwa nini, kila radi ilipopiga, uliacha kukimbia na kutazama juu huku ukitabasamu?” Ah, nilisimama kuangalia juu,” akasema, “kwa sababu Mungu alikuwa ananipiga picha!
Je, mwitikio wetu ni upi wakati dhoruba za maisha zinapokuja au tunapopitia changamoto katika uhusiano wetu na Mungu?
Je, tunainamisha vichwa vyetu huku mvua ikitupiga migongoni, au tunatazama juu, tukijua na kuamini kwamba Mungu yupo tunapomgeukia kwa imani?
Juma hili, tutaangazia baadhi ya miitikio tunayokuwa nayo Mara kwa mara tunapokumbana na changamoto za maisha. Tutaangalia jinsi tunavyoweza kutumia vikwazo vya maisha kuimarisha, badala ya kudhoofisha, uhusiano wetu wa muhimu Zaidi.
Jifunze somo la juma pili ukijiandaa kwa Sabato, Juni 13.