HomeResourcesSabbath School quarterly
Kumjua Mungu
04/04/2026
Somo la Juma Hili
Mwa. 3:1-5, law. 20:26, 1 Sam. 2:2, 1 Yoh. 4:7-19; Mwa. 1:1, Mwa. 2:7, Mt. 1:23, Mt. 28:20.
Fungu la Kukariri
“Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo Uliyemtuma” (#Yohana 17:3#).
Kuwa na ufahamu wazi wa tabia ya Mungu ni msingi wa kuwa na uhusiano thabiti na Yeye. Hii ndiyo sababu, juma hili, tutaangalia kwa makini kile Biblia inachosema kuhusu tabia ya Mungu, tukikumbuka kwamba ni “Ni giza la kutomtambua Mungu, linaloufunika ulimwengu. Watu wanapoteza ujuzi wa tabia Yake. Imekuwa haieleweki, na imetafsiriwa vibaya. Wakati huu ujumbe toka kwa Mungu sharti utangazwe, Ujumbe unaoangaza, kwa mvuto wake, na unaookoa kwa uwezo wake. Tabia Yake ni lazima itambulishwe. Katika giza la ulimwengu huu mng’ao wa utukufu Wake hauna budi kusambazwa, uwe nuru ya wema Wake, huruma Zake na ukweli Wake... ujumbe wa mwisho wa rehema utakaotolewa kwa ulimwengu, kuonesha tabia Yake ya upendo.” — Ellen G. White, Lulu za Usima, uk. 298.
Inaonekana haiwezekani kumweleza Mungu ipasavyo, na kwa hivyo tunachoweza kufanya ni kuelekeza kile ambacho Biblia inasema juu yake. Ijapokuwa hatutawahi kujua, hasa sasa, kila kitu tunachopaswa kujua kuhusu tabia ya ajabu ya Mungu, na tuombe kwamba tunapojifunza zaidi juu Yake, ufahamu wetu na upendo wetu Kwake uzidi kuongezeka, ili hatimaye, tutake kukua karibu Naye ili kuakisi upendo na tabia Yake kwa wengine.
Jifunze somo la juma hili kwa maandalizi ya Sabato ya Aprili 11.