HomeResourcesSabbath School quarterly

Jifunze zaidi

10/04/2026

Mungu anawaita watu Wake kuwakilisha tabia Yake lakini, ili kufanya hivi, tunahitaji kumjua sisi wenyewe. Njia bora zaidi ya kumwona Yeye kwa uwazi, licha ya macho yetu ya kibinadamu yenye dhambi ambayo, mara, nyingi sana huelewa vibaya njia Zake takatifu na kamilifu, ni kupitia kuchunguza Neno Lake, Biblia.

“Upendo wote wa baba ambao umeshuka kutoka kizazi, hadi kizazi kupitia mkondo wa mioyo ya wanadamu, chemchemi zote za huruma ambazo zimefunguka katika roho za wanadamu, ni kama njia ndogo tu ya bahari isiyo na kikomo ikilinganishwa na upendo usio na mwisho wa Mungu. Ulimi hauwezi, kuutamka, kalamu haiwezi kuichora. Unaweza kuutafakari kila siku ya maisha yako; unaweza kuchunguza maandiko kwa bidii ili upate kuyaelewa; unaweza kuleta kila nguvu na uwezo ambao Mungu amekupatia, katika jitihada ya kuelewa upendo na huruma ya Baba wa mbinguni; na bado kutakuwa na milele iliyo mbele zaidi ya hayo, Unaweza kujifunza upendo huo kwa muda mrefu; na bado usiweze kuelewa upana, na urefu, na kimo, na kina cha upendo wa Mungu katika kumtoa Mwana Wake ili afe kwa ajili ya ulimwengu. Milele yenyewe haiwezi kuufunua kikamilifu. Na bado tunapojifunza Biblia na kutafakari maisha ya Kristo na mpango wa ukombozi, mada hizi kuu zitaufungua ufahamu wetu zaidi na zaidi." —Ellen G. White, Testimonies for the Church, gombo la 5, uk. 740.

Masawali ya Kujadili

Muhtasari: Tangu mwanzo wa Uumbaji, Mungu ametamani kuwa katika uhusiano wa karibu nasi. Ingawa ufahamu wetu wa tabia Yake ni shabaha ya mashambulizi ya Shetani, Mungu anajidhihirisha kwetu kwa uwazi zaidi kupitia Neno Lake na kupitia maisha ya Mwanawe, Yesu. Hatimaye, kuwa na picha iliyo wazi na nzuri ya Mungu ni muhimu ikiwa tunataka kuimarisha uhusiano wetu Naye.