HomeResourcesSabbath School quarterly

Mungu ni Upendo

07/04/2026

Upendo pengine ni neno lililozoeleka zaidi katika kutumiwa na Wakristo kuielezea tabia ya Mungu. Yawezekana ikawa ni kwa sababu ya kauli inayomtambulisha Mungu kwenye 1 Yohana 4:8, inayosema, "Mungu ni upendo.” Yohana hakusema, “Mungu anapenda,” bali, “Mungu ni upendo.” Upendo ni tabia Yake, asili halisi inayoonesha Yeye ni nani.

Kwa walio wengi, taswira ya Mungu waliyo nayo inatokana na fasili yao ya upendo, ambayo daima imepotoshwa na pia kuwa na dosari. Badala yake, fasili yetu ya upendo yapasa ijengwe na ukweli kwamba Mungu ni nani na kile anachokifunua juu Yake Mwenyewe kwenye Neno Lake lililovuviwa.

Upendo wa Mungu ni mkamilifu, huru, na una uhusiano wa kina, kama unavyofunuliwa katika mwaliko unaorudiwa wa “kukaa” ndani yake katika 1 Yohana, kwa sababu “Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake” (1 Yohana 4:16).

Mungu ni upendo, na alituumba kwa mfano Wake (Mwa. 1:27) ili kupenda na kutamani upendo. Katika Kiebrania, neno moja kuu la upendo ni hesed. Hilo lafafanua upendo wa agano la Mungu kwa wanadamu, ambao unatia ndani sifa za uaminifu-mshikamanifu, ulinzi, uthabiti na wororo.

Lugha za kale za Kiebrania na Kigiriki hutumia majina mengi tofauti tofauti kurejelea Mungu, majina ambayo yana maana ili kuangazia mambo mbalimbali ya tabia nzuri ya Mungu. Hapa kuna mifano miwili tu:

Hatimaye, onesho kuu zaidi la upendo wa Mungu linafunuliwa kupitia zawadi ya Mwanawe kwa dunia hii (Yohana 3:16) ambaye alikufa kwa ajili ya wenye dhambi (Rum. 5:8). Mungu angeweza kuwanyima wanadamu jambo hili lakini kwa sababu ya upendo Wake mkuu, usio na upeo, usio na ubinafsi, Mungu alimtuma Yesu duniani ili tuweze kuchagua kwa hiari kuitikia upendo Wake, uliofunuliwa katika kifo Chake ambacho alikufa kama mbadala kwa ajili yetu. Si tu kwamba Yesu aliziba ufa ambao dhambi iliuweka kati yetu na Mungu (Isa. 59:1, 2), Aliishi ili kutuonesha tabia kamilifu ya Mungu ya upendo (Yohana 14:9, Ebr. 1:3) na kuwavuta watu wote Kwake (Yohana 12:32).