HomeResourcesSabbath School quarterly
Kuwa na Imani
16/05/2026
Somo la Juma Hili
Marko 8:11,12; Mt. 15:21-28; Lk. 7:1-10; Efe. 2:8; Ebr. 11; Ufu. 14:12.
Fungu la Kukariri
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana (#Ebr 11:1#).
Mtu fulani aliwahi kusema, Imani ni kama WiFi, haionekani lakini ina uwezo wa kukuunganisha na kile unachohitaji. Hakuna shaka kwamba pasipo imani, kusingekuwa na uhusiano na Mungu.
Imani yako ikoje leo? Je, imani yako kwa Mungu imewahi kuyumbayumba? Huenda umepata uzoefu wa kitu ambacho kimekupa changamoto kiasi cha kushindwa kuelewa jinsi ya kusonga mbele katika uhusiano wako na Mungu. Au imani yako ni kama ua la waridi ambalo linachipuka kutoka katika shina la kijani na kuwa chipukizi jembamba ambalo mara huchanua na kuwa ua lenye rangi nzuri na kukijaza chumba kwa harufu nzuri isiyoweza kusahaulika? Kwa hakika, imani huonesha uhalisia wa kile tunachokitarajia; ni bayana ya mambo tusiyoweza kuyaona (Ebr. 11:1 tafsiri ya kutoka NLT). Si kitu ambacho tunaweza kukitengeneza sisi wenyewe, kwa maana Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani (Rum. 12:3). Imani ni karama ya Mungu (Efe. 2:8,9), na hata hapo, imani yetu kwa Mungu inawezekana kwa sababu tu ya kile ambacho Mungu tayari anafanya ndani yetu na kwa ajili yetu.
Juma hili hebu tuchungue mada ya imani: cha kufanya na mashaka na kutokuamini; kile ambacho, kwa mujibu wa Yesu, imani imara inafanana nacho; na maana ya kuwa na imani ya Yesu.
Jifunze somo la juma hili ili kujiandaa kwa ajili ya Sabato, Mei 23.