HomeResourcesSabbath School quarterly

Yesu Anaiona Imani Yetu

18/05/2026

Kwa vile tu tunajiita wafuasi wa Yesu haimanishi kuwa hiyo inaifanya imani yetu kuwa imara. Kwa kweli, kuna watu walidai kuamini, lakini Yesu alitambua kile halisi kilichokuwa myoyoni mwao (Yohana 2:23-25).

Katika Mariko 9 tunasoma habari za mtu aliye kuja kwa Yesu ili kwamba Yesu amtoe mwanawe pepo, lakini aliyeweza tu kuitia ujasiri wa kutosha imani yake na kusema Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu! (Mk. 9:24).

Katika kila moja ya mazungumzo haya, Yesu aliona imani ya watu, au kupungua kwake, na kufanya miujiza kama matokeo ya imani hiyo au kwa ajili ya kuiimarisha.

Ingawa Roho Mtakatifu hutuhimiza kuamini, adui wa roho anatutaka tuwe na mashaka na kuondolea mbali uhusika wa Mungu katika maisha yetu. Hali ya kutokuamini inayooneshwa ndani ya roho ina nguvu ya ushawishi. Mbegu za mashaka ambazo wamekuwa wakizipanda zitaleta mazao yake lakini imewapasa kuendelea kung'oa kila mzizi wa kutokuamini. Wakati mimea hii yenye sumu inapong'olewa, inakoma kukua kwa uhitaji wa virutubishi kwa maneno na matendo. Roho inapaswa kuwa na mimea ya thamani ya imani na upendo iliyopandwa katika udongo wa moyo na kutawazwa hapo.—Ellen G. White, Faith and Works, uk. 17.

Tunapokuwa na mashaka juu ya Mungu, tabia Yake au Neno Lake, tufanyeje? Mungu hapuuzii au kuiepuka mantiki ya mwanadamu, kwa kuwa alituumba kwa sura yake, na anatualika kuzungumza Naye, kama alivyofanya na Ibrahimu, Musa na Ayubu. Mungu anatualika kujifunza kufanya kazi ndani ya mifumo yake mikubwa isiyo na kikomo ya busara, hata kama mahali fulani inatupasa kujisalimisha kwa kile tusichokielewa kikamilifu.