HomeResourcesSabbath School quarterly
Harakati za Maisha
31/05/2026
Lilikuwa juma lenye shughuli nyingi sana. Ingawa alijua kuna mambo mengi ya kufanya kabla ya sabato, yaliyokuwa ya dharura yaliingilia yaliyokuwa ya muhimu, na kabla hajalijua hilo, jua lilikuwa limezama. Familia ilishiriki chakula maalum cha usiku wa Ijumaa na ibada pamoja.
Lakini asubuhi ya Sabato ilipowadia akaamka mapema, hakuweza kujizuia kuona choo kilichokuwa kichafu, ambacho alikisafisha. Kisha akaona kuwa mwanawe mdogo alikuwa amekojoa kitandani, hivyo akatupa mashuka yake kwenye mashine ya kufulia pamoja na nguo nyingine. Alipokuwa akiandaa kifungua kinywa Kwa ajili ya familia yake, aligundua kuwa hakukuwa na kitindamlo kwa chakula cha mchana, hivyo akaoka mkate wa ndizi haraka. Akaona kuwa mume wake alihitaji shati lililopigwa pasi kwa ajili ya kwenda kanisani, hivyo akalifanya hilo pia, kisha akakunjua nguo na kwenda kutupa takataka nje.
Kisha akagundua. Ni Sabato—siku, ninayoipenda, kuliko siku nyingine yoyote! Lakini hapa niko, nikifanya kazi hizi zote na
kuruhusu mambo haya kunivuta kutoka kwenye maana halisi ya Sabato —kusogea karibu na Mungu.
Kwa muda mfupi akili yake ilianza kuhalalisha matendo yake—haya yote yalikuwa mambo yaliyohitajika kufanywa. Je, kweli yalihitajika? Alitambua kuwa alikuwa akitenda kama Martha, “alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi" (Luka 10: 40), lakini maneno ya Yesu yakagonga akilini mwake: “Unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi. lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa’ ” (Luka 10:41, 42), Fungu lile jema. Kuketi miguuni pa Yesu kwa upendo wa dhati Kwake—si tu siku ya Sabato, bali kila siku. Hakuwa amechagua hilo asubuhi hiyo.
Alimpenda Mungu, lakini ilikuwa rahisi kusahau kwamba Alikuwa amempa Sabato kama zawadi ya wakati ili kuimarisha uhusiano wao. Machozi ya kimya yalimtiririka machoni alipokuwa amesimama jikoni.
Kusudi la mfano huu si kuangazia kile tunachopaswa au tusichopaswa kufanya siku ya Sabato; bali ni kutukumbusha kwa nini ni muhimu kutambua mambo yanayodhoofisha au kuvunja uhsiano wetu na Mungu. Mioyo yetu inapohisi maumivu ya dhambi na utengano na tukamwita, Yesu yuko karibu sana (Zab. 53:2). Katika mikono Yake iliyo na damu, anashika vazi jeupe. Anaona machozi yetu ya toba na kuondoa nguo zetu chafu. Kisha anatufunika kwa vazi Lake safi la haki. Utakatifu Wake unafunika dhambi zetu zilizoungamwa—kabisa na kwa ukamilifu. Tunaweza kuosha vazi letu katika damu Yake (Ufu. 7:14).