HomeResourcesSabbath School quarterly

Neema ya Kutosha

03/06/2026

Tunapohisi uzito wa dhambi zetu na kumruhusu Roho Mtakatifu atuongoze hadi msalabani, tunapaswa kuomba msamaha wa Mungu, tukijua kwamba “Bwana amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili” (Zab. 103:8). Aya hii ilitamkwa na Mungu Mwenyewe (Kut. 34:6) baada ya taifa Lake teule kumhuzunisha.

Ukweli kwamba Bwana ni mwenye rehema na neema, si mwepesi wa hasira, bali mwingi wa rehema, ndiyo sababu hasa Yesu alikufa msalabani—ili uhusiano wetu na Mungu urejeshwe kuwa sawa tena.

Ni wakati tunapokuwa tayari kukiri na kuungama dhambi zetu; tunaposema, Ee Bwana, niko hapa tena .... uniwie radhi mimi mwenye dhambi! (Luka 18:13), ndipo Yesu—ambaye tayari amekuwa akifanya kazi ndani yetu na kwa ajili yetu pamoja na Roho Mtakatifu hata kabla hatujamwita—anapoona mzigo huo na kuundoa kwetu. Mizigo yetu huondolewa pale Kalvari, na Yesu hakika yuko karibu sana tunapomjia, na hata kabla ya hapo, hututafuta kama Mchungaji Mwema na husimama mlangoni akibisha (Ufunuo 3:20). Tusiendelee kukaa mbali na Msalaba, tukimtazama Mungu kutoka mbali. Hebu tukimbilie kwa Yesu na kubadilishana dhambi zetu na mizigo yetu kwa haki Yake (Zekaria 3:4)

`Polepole soma aya zifuatazo. Andika kwa maneno yako mwenyewe kile zinachokwambia juu ya neema ya Mungu kwako:

“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23)

“Na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu” (Warumi 5:20, 21).`