HomeResourcesSabbath School quarterly

Toba ya Kweli

02/06/2026

Ulimwengu wa kidunia unatujaza kwa ujumbe wa kujitegemea, kuendekeza tamaa, na kujitukuza—kinyume kabisa na kanuni za Ufalme wa Mungu. Cha kuvutia ni kwamba maneno ya kwanza yaliyoandikwa katika Biblia kutoka kwa Yohana Mbatizaji na Yesu yalifanana. Yohana alisema, “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 3:1, 2). Yesu alisema, “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injil” i(Marko 1:14, 15; tazama pia Luka 24:46, 47). Yesu na Yohana waliwataka waliokuwa wakisikia watubu kwa sababu Ufalme wa mbinguni ulikuwa umekaribia. Je, inawezekana kwamba ujumbe huu bado ni muhimu kwetu leo?

Wema na fadhili za Mungu hutuelekeza katika toba (Warumi 2:4), Toba inahusisha hatua mbili: (1) maumivu ya kweli na huzuni kwa ajili ya dhambi zetu; na (2) uamuzi wa dhati wa kuziacha dhambi. Katika Biblia, toba karibu kila mara inaunganishwa na msamaha. Tunapotubu kutoka moyoni, Mungu husamehe. Ni hivyo tu (1 Yohana 1:9, Ufunuo 3:19). “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba” (2 Petro 3:9). Tunapoziandaa roho zetu kwa ajili ujio wa Yesu Kristo mara ya pili, Mungu anatupa muda wa kurekebisha mambo yetu na Yeye.

Yesu aliteseka, akafa, na akafufuka ili kwamba tunapotubu, neema Yake iweze kufanya muujiza katika maisha yetu. Tofauti na dunia, ambayo hutwambia kuwa tuko sawa jinsi tulivyo Mungu hutusihi tumgeukie kwa toba na imani (Matendo 20:21), tukijiweka kikamilifu mikononi Mwake ili aweze kututakasa na kutufinyanga kwa uzuri katika mfano Wake, ili tumshuhudie (Yohana 15:2, 8). Kisha tunakua na kuzaa matunda yanayoendana na toba (Mathayo 3:8).

Hakuna toba ya kweli isiyoleta mabadiliko. Haki ya Kristo siyo vazi la kufunika dhambi ambazo hazijaungamwa wala kuachwa; ni kanuni ya maisha inayobadilisha tabia na kuongoza mwenendo.—Ellen G. White, The Desire of Ages, uk. 555, 556.