HomeResourcesSabbath School quarterly
Shiriki Habari Zake
13/06/2026
Somo la Juma Hili
Mt 28:18-20, 2 Pet. 3:18, 1 Pet. 3:8-15, Hosea 7, Zekaria 10.
Fungu la Kukariri
“Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao” (#Isaya 50:4#).
Ilikuwa asubuhi ya Sabato yenye shughuli nyingi kwa Mchungaji G. Alikuwa ameamka mapema, akijiandaa kwa ajili ya Shule ya Sabato na mahubiri, na pia alikuwa akiendesha mfululizo wa mikutano ya injili alasiri. Alichukua funguo zake, akatoka haraka mlangoni, na kuondoka kwa kasi.
Aliendesha katika barabara yenye msongamano wa magari mjini, akikasirishwa na watu wengi waliokuwa barabarani asubuhi ya jumamosi, wakionekana kumchelewesha kwenda kanisani. Walikuwa wanaelekea wapi wote hao? Kisha, ghafla, gari moja likakatiza mbele yake. Alikanyaga breki kwa nguvu na kukunja ngumi kwa hasira na kumfokea dereva.
Hatimaye, Mchungaji G. aliwasili kanisani. Aliposimama ili kufundisha somo, macho yake yalikagua darasa lake na yakasimama katika sura ambayo haikuwa ngeni: dereva wa gari aliyemkasirikia dakika 20 zilizopita.
Baadaye, mshiriki mmoja wa kanisa alipomtambulisha dereva huyo kama mtu asiye Mwadventista aliyekuwa akitembelea ndugu zake, Mchungaji G. alitambua tena kwamba kila kutendeana, iwe ni kwa watu tunaowajua au wageni, kunapaswa kujaa upendo unaotiririka kutoka katika uhusiano wa kudumu na Mungu. Huwezi kujua ni kwa namna gani matendo yako, hasa kama muumini, yanaweza kuwa na athari kwa wengine.
Jifunze somo la juma hili ukijiandaa kwa Sabato, Juni 20.