HomeResourcesSabbath School quarterly
Kutokana na Mafuriko
14/06/2026
Yesu alitupa agizo la kushiriki ujumbe Wake kwa ulimwengu: “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi.” Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato ni kuwafanya watu kuwa wanafunzi, ambao nao watawafanya wengine kuwa wanafunzi. Kwa njia hiyo, sote tunatangaza injili ya milele na ujumbe wa malaika watatu (Ufunuo 14:6—12) ili kuandaa dunia kwa ajili ya kurudi kwa Yesu kunakokaribia.
Kila mtu aliyepokea maisha mapya katika Kristo ameitwa kushuhudia. Hata hivyo, mara nyingi watu hufikiri kuwa kushuhudia ni jambo gumu au wasilotaka kulifanya. Unaweza kujiona ukihubiri mtaani au ukitoa somo gumu la Biblia, na ukatikisa kichwa chako: “Si mimi! Haiwezekani! Mimi ni mtu mkimya; kushuhudia si eneo langu nililokirimiwa.”
Hata hivyo, ushuhudiaji wa kweli mara nyingi hutokana na kuwa shahidi wa kile ambacho Mungu anafanya katika maisha yako, kuona kile Anachokufundisha unapokua ndani Yake, na kisha kushiriki tu uzoefu wako pamoja na wengine. Mungu ni mwema sana, na kile alichokifanya kwetu ndiyo habari njema zaidi ambayo dunia hii inaweza kusikia. Hatuwezi wala hatupaswi kunyamaza! Amekukomboa; amekuita kwa jina lako—wewe ni Wake. Je, kuna habari njema zaidi kwa mtu yeyote mahali popote?
Ingawa wanafunzi wa kanisa la awali hawakuwa wamesoma katika shule za Kiyahudi au wenye ufasaha katika mapokeo ya simulizi, bado tunaweza kujifunza kutoka kwao.
Petro na Yohana waliendelea kutangaza, “ ‘Maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia ” (Mdo. 4:20). “Walikuwa pamoja na Yesu” (Mdo. 4:13) na walilazimika kushiriki. Roho Mtakatifu aliwapa ujasiri na nguvu ya ushawishi katika maneno yao.