HomeResourcesSabbath School quarterly

Warudisheni

18/06/2026

Wote tumewahi kupitia nyakati za udhaifu au kuyumba katika kutembea kwetu na Mungu—mabonde ambayo mioyo yetu haikuaminika au ambapo tulikuwa vuguvugu kwa muda mrefu. Ni kitu gani kilichokurejesha katika uhusiano wa kudumu pamoja naye?

Zekaria 10 inashiriki ujumbe mzuri kuhusu Mungu kuwarudisha watu Wake kwake. Soma sura hii sasa hivi polepole na uandike ujumbe mkuu.

Kwa namna halisi, kujua jinsi ya kuhusiana na kuwasiliana na mpendwa aliyeacha uhusiano wake na Bwana kunaweza kuwa changamoto. Unaweza kujiuliza jinsi mambo yanavyoweza kugeuka; unaweza kujiuliza jinsi ya Kuwasiliana naye sasa kwa kuwa ana mtazamo tofauti; na unaweza kujisikia kufadhaika na kutokuwa na msaada kutokana na maamuzi mabaya ambayo bado anaweza kuwa anayafanya. Mawazo haya yataathiri kila wakati jinsi unavyomtendea mpendwa wako, na ndiyo maana ni muhimu sana kuishi na kuzungumza kutokana na wingi wa muda wako binafsi na Mwokozi wako.

Ushuhuda wa maisha yako, matendo yako, maneno yako, na maombi yako kwa ajili ya mwenzi au mtoto aliyekengeuka unaweza kubadilisha kabisa maisha na mustakabali wao. (Soma katika Luka 22:31, 32 na Yohana 21:15—17 jinsi maombi ya Yesu kwa Petro yalivyobadili maisha yake ya baadaye.) Kabidhi huzuni yoyote, hukumu, au shutuma unazoweza kuhisi juu yao, na badala yake mwombe Mungu abadilishe hisia hizo kwa upendo ambao ni Yeye tu awezaye kutoa. Mwombe Mungu akufunike kwa tabia Yake ili uweze kuonesha mtazamo wa upendo usio na ubinafsi. Kumbuka kwamba “hakuna mvuto mwingine unaoweza kuizunguka nafsi ya mwanadamu mwenye nguvu kama mvuto wa maisha yasiyo na ubinafsi. Hoja yenye nguvu zaidi inayoungana na injili ni Mkristo mwenye upendo na anayependeka.”—Ellen G. White, The Ministry of Healing, uk. 470.

Kupitia mfano wa “maisha yetu thabiti yanayowaelekeza wengine kwa Kristo, wale waliomkataa Kristo wataona ndani yetu kitu ambacho kinatoka kwa Mungu tu. Wataona amani ipitayo ufahamu, upendo usiokata tamaa, na tumaini linaloamini hata kinyume na hali ilivyo. Upendo wa Mungu kwetu na kwa wapendwa wetu hautetereki kamwe. Tunaweza kutoa upendo huu, ambao tunaupokea kila siku, kwa wale wanaotuzunguka.