HomeResourcesSabbath School quarterly
Mwana Mpotevu
17/06/2026
Wengi wanajua kwa uzoefu uchungu na maumivu ya kuwa na mtoto ambaye—licha ya kulelewa katika nyumba yenye msingi imara wa kiroho—amechagua kuacha uhusiano wake na Bwana.
Zaidi ya hayo, tunasoma kwamba Raheli, bibi yake Efraimu, analia kisitiari kwa sababu Efraimu ameacha uhusiano wake na Bwana (Yer. 31:15). Bwana anajibu huzuni yake kuu kwa maneno haya katika Yeremia 31:16, 17: “ “Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; Maana kazi yako itapata thawabu, nao watakuja tena toka nchi ya adui. Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema Bwana; na watoto wako watarejea hata mpaka wao wenyewe.’ ”
Kupitia kisa cha Efraimu, tunajifunza kwamba daima kuna tumaini, kwa sababu Mungu hakati tamaa. Ingawa Anawakemea watu Wake waliopotoka mara kwa mara, huruma ya Mungu haikomi na ujumbe Wake katika sura hii unaendelea (Tazama Yer. 31:20).
Tunaweza kuhisi maumivu makubwa, kufadhaika na kukatishwa tamaa, au hata kusema mambo mabaya kuhusu wale walio karibu yetu ambao wameacha uhusiano wao na Mungu. Hata hivyo, Mungu anatukumbusha kwamba hajamsahau mtoto aliyetanga mbali—kamwe! Mawazo ya Mungu juu ya mtu kama huyo si ya muda mfupi tu, bali ni ya dhati na ya kweli. Kwa kweli, Mungu anasema kwamba moyo Wake unamwonea shauku mtu wa aina hiyo. Anatamani arudi Kwake, na rehema Zake ni nyingi.